7. Uchunguzi Hakiki ni nini?

Ilitumwa Februari 5, 2020

Ziara za uchunguzi hakiki ni muhimu katika kutathmini athari na vihatarishi vilivyopo kabla ya FCS kuwekeza fedha na muda wake. Waombaji wote wapya ambao wamefuzu mchakato wa mchujo watafanyiwa uchunguzi hakiki (Isipokuwa wale watakaofaulu kupewa msamaha kama ilivyooneshwa kwenye ukurasa wa kudhibiti vihatarishi). Wakati wa Uchunguzi hakiki tume ya FCS, itafanya uchunguzi wa kufika na kuona kwa macho hali halisi ya waombaji wote wanaotarajiwa kufadhiliwa. Zoezi hili linalenga kuhakiki ukweli wa taarifa za wafadhiliwa watarajiwa, kuchunguza na kutathmini uwezo wa ndani wa asasi sambamba na mahusiano ya asasi na wadau wake, wanufaika na mamlaka za serikali za mitaa. Katika kutekeleza zoezi hili pamoja na masuala mengine, washauri watatumia dodoso la Uchunguzi hakiki litakalotolewa na FCS. Zoezi hilo litafanywa na kampuni ambayo itateuliwa kupitia mchakato wa zabuni wa kawaida. Matokeo ya zoezi la Uchunguzi hakiki yatawasilishwa kwenye kikao cha menejimenti na ripoti zitapelekwa Idara ya Fedha na Uendeshaji.

jQuery(document).ready(function($) { $.post('https://thefoundation.or.tz/wp-admin/admin-ajax.php', {action: 'wpt_view_count', id: '3492'}); });
Category: Swahili