6. Ni ukaguzi gani wa lazima na hati gani zinahitajika wakati wa kupeleka maombi yako FCS?
Ilitumwa Februari 5, 2020
Yafuatayo ni vitu vya lazima kukaguliwa.
Sifa za mwombaji kulingana na vigezo na masharti ya FCS
Fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu
Katiba ya ASASI
Hati ya Usajili wa ASASI
Taarifa ya Benki
Asasi yoyote ambayo iko kwenye orodha ya asasi zilizowekewa vikwazo au haijaweza kuwasilisha nyaraka zote za lazima zilizoorodheshwa hapo juu itaondolewa kwenye hatua ya mchujo.