5. FCS ina aina ngapi za matangazo ya wito wa kutuma maombi ya ruzuku/maandiko ya miradi?

Ilitumwa Februari 5, 2020

 FCS itatoa aina kuu mbili za matangazo ya wito wa kutuma maombi/maandiko mradi kama ilivyooneshwa hapa chini:

i) Tangazo la jumla la kutuma maombi: FCS itatoa angalau tangazo mmoja la kutaka waombaji wawasilishe maombi kama ilivyoainishwa kwenye mpango wa kila mwaka kulingana na matokeo ya maeneo muhimu ambayo ni utawala bora na Ustawi wa Jamii /Maendeleo ya Kiuchumi. Tangazo la jumla litatolewa mwezi Novemba kila mwaka au mwezi Januari wa mwaka unaofuatia au litatolewa kulingana na upatikanaji wa fedha na kwa kuzingatia maamuzi ya wakati huo ya menejimenti.

ii) Tangazo la kutuma Maombi maalum: Hili ni tangazo linalotolewa kwa lengo la kuwezesha utekelezaji kwenye masuala maalum au kutoa mwitikio wa haraka kwa masuala yanayoibuka yenye masilahi ya kitaifa kwenye maeneo ya utawala bora na Mahitaji ya maisha/Maendeleo ya Kiuchumi. Tangazo maalum pia litatolewa kwa lengo la kuwavutia waombaji wa ruzuku kwenye miradi maalum ambayo iko nje ya fedha za mfuko mkuu. Wakati mwingine pia na kwa kuzingatia mahitaji maalum yanayoweza kujitokeza, FCS inaweza kuwasiliana na asasi fulani ili kutatua masuala muhimu au kutekeleza kazi maalum. Namba za utambulisho wa Mradi zitaainishwa kwa kuzingatia dirisha la ruzuku na jina la wafadhili maalum wanaogharamia programu hiyo. Katika matangazo yote mawili, maombi ya Ruzuku hufanywa kupitia Fomu maalum iliyotolewa ambayo inapatikana kwa lugha zote mbili yaani katika Kiswahili au Kiingereza na hivyo, asasi inaweza kuomba kwa kutumia lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Fomu hiyo ina maelekezo ya kina yanayofafanua kuhusu nini kinachohitajika. Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa kujaza moja kwa moja kwenye mtandao au kwa kujaza Fomu ya karatasi. Waombaji wa ruzuku watahimizwa zaidi kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao na kuhakikisha kuwa viambatisho vyote muhimu kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye tangazo vimeambatanishwa. Hakutakuwa na tofauti ya aina ya viambatisho vilivyowasilishwa na waombaji kwa njia ya mtandao na wale watakaotumia Fomu za karatasi. FCS itatoa siku kati ya 21 hadi 30 kwa waombaji kuwasilisha maombi yao. Hata hivyo, kutokana na suala la ucheleweshaji wa fedha, menejimenti itaamua ni wakati gani muafaka wa waombaji wawasilishe maombi yao.

jQuery(document).ready(function($) { $.post('https://thefoundation.or.tz/wp-admin/admin-ajax.php', {action: 'wpt_view_count', id: '3490'}); });
Category: Swahili