1. Kuna aina ngapi za ruzuku inayotolewa na FCS?

Ilitumwa Septemba 16, 2019

Zifuatazo ni aina tatu za ruzuku zinazotolewa na FCS: –

  1. Ruzuku ya Kimkakati: Hii ni ruzuku kubwa zaidi ambayo FCS inatoa kwa Mitandao ya Asasi za kiraia, Mashirika Mwamvuli ya Asasi za Kiraia yaliyo makini na yenye kufanyakazi kwa mafanikio na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi ngazi ya Kitaifa na zenye rekodi nzuri ya kusimamia fedha na kuleta matokeo yanayoonekana kote Tanzania. Mashirika ya aina hii yanapewa ruzuku kama “Viongozi wa Klasta” yaani, kwa mfano – kiongozi kwenye kundi la Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma au Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii; kiongozi kwenye kundi la Utetezi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vibaya vya kimila nk. Mashirika haya yanapanga programu zao kwa namna ambayo wataweza kufanya kazi na AZAKi za kijamii zinazofanya kazi kwenye sekta na maudhui yao na kutumia mambo waliyojifunza kutoka ngazi ya jamii kushawishi utetezi kwa ngazi ya kitaifa, wakati huo huo wakitumia mambo waliyojifunza ngazi ya kitaifa kuyapeleka kusaidia kufanikisha miradi ngazi ya jamii.
  2. Ruzuku ya Kati: Aina hii ya ruzuku ndio imebeba sehemu kubwa ya kazi ya utoaji ruzuku ya FCS. Aina hii ya ruzuku inalenga mashirika ya kiwango cha kati ambayo yameonesha uwezo mubwa katika kusimamia mradi na matumizi ya fedha.
  3. Ruzuku ya Ubunifu: Ruzuku ya ubunifu imeyalenga mashirika ambayo yatatekeleza mikakati bunifu ya kuleta ufumbuzi na utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii kulingana na matokeo tarajiwa ya FCS. Dirisha hili pia linatoa fursa kwa asasi ndogo na mpya pamoja na zile changa ambazo zina mawazo bora ya kusaidia kuboresha changamoto za utawala maeneo yao. Pia inajumuisha mashirika ambayo yatapata ruzuku chini ya Tsh 50,000,000 / = na ambayo wanakusudia kutekeleza miradi nchini kote lakini kwa kufuata maudhui ya maeneo ya matokeo yaliyopangwa na FCS.
jQuery(document).ready(function($) { $.post('https://thefoundation.or.tz/wp-admin/admin-ajax.php', {action: 'wpt_view_count', id: '3473'}); });
Category: Swahili