Bwana Francis Kiwanga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society tangu mwezi Machi 2015. Ni mtaalamu wa masuala ya asasi za kiraia na sheria – mwenye maono, mtazamo chanya, muwazi na mwenye uzoefu katika ngazi za juu za menejimenti, ana ujuzi mkubwa kwenye masuala ya usimamizi na uelewa mpana wa ajenda ya maendeleo, asasi za kiraia, serikali na sekta binafsi nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki. Bwana Francis ana uzoefu wa zaidi ya miaka 17.
Huko nyuma alifanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Kampuni ya Consulting Matrix- inalojihusisha na masuala ya kutoa ushauri wa sheria, kodi na utawala lililopo Arusha ambalo yeye ni mmoja wa waanzilishi. Kama wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania amefanya kazi kubwa kwenye maeneo ya sheria, utawala na Haki za binadamu kwa zaidi ya miaka 8.
Anauzoefu na ametoa ushauri wa kitaalumu kwa mapana juu ya Usimamizi wa Ruzuku na uhamasishaji wa kupata rasilimali, uongozi wa makampuni na biashara za kijamii, utawala bora, uchambuzi wa sera za kijamii, mikakati ya kupambana na rushwa na mifumo ya uwajibikaji, Ushiriki wa umma na mchakato wa kidemokrasia. Bwana Kiwanga ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara, (MBA) kutoka Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) Arusha na Shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Ni mjumbe kwenye mashirika mbalimbali ya kitaaluma na bodi za taasisi kama vile Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ,East Africa Association of Grantmakers (EAAG) na Africa Philanthropy Network (APN).