WITO WA MAOMBI YA RUZUKU MAALUM KWA MASHIRIKA, JUMUIYA NA ASASI ZA KIRAIA – ZANZIBAR
UTANGULIZI
Foundation for Civil Society (FCS) ni shirika huru la kimaendeleo, la Kitanzania lisilolenga kupata faida, ambalo hutoa ruzuku na kujenga uwezo wa Asasi za Kiraia za Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake FCS
imechangia kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha uwezo wa sekta ya kiraia nchini Tanzania bara na Visiwani.
Foundation for Civil Society ikishirikiana na Search for Common Ground – Tanzania, wanatekeleza kwa pamoja mradi wa DUMISHA AMANI-Zanzibar kwa muda wa miezi 18 kuanzia mwezi March 2021.
Kijiografia mradi huu unatekelezwa Unguja na Pemba katika Mikoa na Wilaya zote, ili kuimarisha ushiriki wa wanajamii katika utatuzi wa migogoro kupitia njia shirikishi, majadiliano na midahalo ili kufikia
maafikiano katika jamii na hivyo kudumisha amani Zanzibar.
MALENGO MAKUU YA MRADI
Malengo mahsusi ya mradi huu unaotekelezwa baina ya FCS na SEARCH ni pamoja na,
- Kujenga uwezo wa wadau mbalimbali katika jamii wakiwemo viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wanasiasa, asasi za kijamii na wengineo kuwa wasuluhishi mahiri wa kuleta amani katika
jamii zao - Kuhimiza midahalo, majadiliano ya amani na mashirikiano baina ya wadau mbalimbali kama vile,
serikali, viongozi wa dini, na wanajamii ili kuzuia kutokea kwa migogoro. - Kuongeza mwamko na kuleta tija katika jamii juu ya juhudi za kuzuia migogoro na usuluhishi kwa
njia ya amani.
Ili kufikia malengo mahususi ya mradi tajwa hapo juu, FCS na SFCG inazialika Asasi za Kiraia na Jumuiya
za wazawa zilizosajiliwa, zenye mlengo na ujuzi wa kufanya miradi kwenye eneo la ujenzi wa amani na
utatuzi wa migogoro kutoka Unguja na Pemba kuomba ruzuku. Kwa maelezo zaidi juu ya huu wito wa maombi bofya hapo chini - Wito wa maombi ya ruzuku
- Kielelezo cha andiko la mradi