Hapa Rushwa Haikubaliki 

Foundation for Civil Society (FCS) ni taasisi isiyovumilia aina yoyote ya vitendo vya rushwa kuanzia katika shughuli zake za ndani mpaka kwa asasi, mashirika na wadau inaoshirikiana nao.

Kama umeshuhudia tukio au vitendo vyovyote vya rushwa kwa mtu au wadau wanaoshirikiana na mfanyakazi, asasi au mtoa huduma yeyote anaefanya kazi na Foundation, tafadhali wasiliana na Mkurugenzi Mtendaji na utoe taarifa mapema kupitia barua pepe ya siri ifuatayo: 

whistleblower@thefoundation.or.tz 

FCS ina sera isiyovumilia vitendo vya rushwa ambayo hulinda watoa taarifa wote. Tafadhali tushirikiane kupambana na rushwa.

unaweza kujaza fomu ya kutoa taarifa  za tukio au vitendo vyovyote vya rushwa