Sisi ni nani

Kwasasa ni moja ya Taasisi kubwa, na chanzo kikuu cha ufadhili kwa AZAKi za Kitanzania – kwahiyo, FCS inaziwezesha moja kwa moja AZAKi na wananchi kuwa chachu muhimu na mstari wa mbele kushawishi utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania na maisha bora kwa watu wote. Kwahiyo, FCS ni mfadhili na mwezeshaji wa kati wa AZAKi nchini Tanzania na anayelenga kuwezesha ushiriki mzuri wa AZAKI kwenye jitihada za kupunguza umasikini kwa njia ambazo zinaambatana na juhudi za serikali na Washirika wa Maendeleo(DPs)kuelekea kupunguza umasikini kama ilivyopangwa kwenye miongozo mikuu ya maendeleo ya Tanzania: Dira ya Taifa ya Maedeleo ya 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016-2020.

Related News