Nani anaweza kuomba ruzuku

NANI ANAWEZA KUOMBA RUZUKU

Foundation inaweza kutoa ruzuku kwa mashirika ya ndani ambayo yameanzishwa kwa malengo yasiyo ya kupata faida binafsi. Hata kama shughuli ambayo unaombea ruzuku ni ya kutoa msaada au uhisani, hautastahili kupewa ruzuku hadi pale katiba ya shirika lako itasema wazi aina ya msaada au uhisani ambao shirika lako limepanga kuutoa kwa jamii. Kama unadhani shirika lako linaweza kuathiriwa na sharti hili, tafadhali pata ushauri kutoka Foundation kabla ya kutuma maombi ya ruzuku. Taasisi zifuatazo zina sifa ya kuomba ruzuku ya Foundation for Civil Society:

 1. Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO);
 2. Vyama vya kitaaluma;
 3. Vyama vya wafanyakazi
 4. Mashirika ya vyombo vya habari (kwa miradi yenye malengo ya kijamii na siyo kupata faida) 
 5. Asasi za kidini (FBO) – (kwa miradi yenye malengo ya kijamii na siyo kutangaza dini/injili) yao.
 6. Vyama vya ushirika (miradi yenye malengo ya kijamii siyo kupata faida)

MAENEO AMBAYO FCS  HAITOI RUZUKU 

Foundation haitoi ruzuku kwenye maeneo yafuatayo:

 • Matoleo/shukrani na ufadhiliwa wa masomo
 • Miradi au shughuli zilizo nje ya Tanzania.
 • Miradi au shughuli ambazo tayari zimekamilika
 • Miradi ambayo inatoa ruzuku kwa mashirika mengine.
 • Posho ya asante kwa wafanyakazi wa kuajiriwa
 • Shughuli za kuingizia kipato/ mikopo midogo midogo
 • Maombi kutoka kwa wataalamu wa kuchangisha fedha au Wataalamu-washauri wanaofanya kazi kwa niaba ya mashirika
 • Mtu mmoja mmoja
 • Vyama vya siasa.
 • Miradi inayotangaza dini fulani, kabila/kundi fulani, rangi fulani au utamaduni fulani
 • Biashara za sekta binafsi (isipokuwa kama hazitoa faida binafsi)
 • Mashirika ambayo yana madeni makubwa.
 • Semina au Makongamano ya kujitegemea
 • Semina, isipokuwa kama ni sehemu ya shughuli zilizopangwa na zinahusiana na matokeo tarajiwa
 • Gharama zisizotarajiwa (dharura).

Nashauri pia sera ya kutokuvumilia rushwa  iwekwe hapa

Unahitaji ufafanuzi zaidi?

Kama unapenda kupata ufafanuzi zaidi juu ya ruzuku na taratibu zetu tafadhali tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa mara au wasiliana na Meneja wa Programu wetu kupitia: fuhadi@thefoundation.or.tz.

Related News