Foundation for Civil Society ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa mwaka 2002 na kuanza utekelezaji mwaka 2003, ikiwa ni taasisi yenye kutoa ruzuku na kuimarisha uwezo kwa Asasi za kiraia nchini Tanzania kutekeleza miradi yenye kuboresha hali za wananchi.
Mnamo mwezi Septemba 2021, FCS ilizindua Mpango Mkakati wake wa mwaka 2022 – 2026. Mwaka huu FCS inaanza kutekeleza mpango mkakati huo wa miaka mitano ili kuchangia juhudi za kuboresha maisha ya watanzania. Ili kuweza kutekeleza adhma hii, FCS inawaalika wadau wote katika warsha ya upashanaji habari za shughuli za FCS kwa ajili ya kutangaza utaratibu mpya wa kufanya kazi na wadau mbalimabili wakiwemo vikundi, watu binafsi, pamoja na mashirika mbalimbali ya kiraia yenye kuleta chachu ya mabadiliko bara na visiwani.
Warsha hii itafanyika siku ya Jumanne tarehe 17/05/2022 kwa kanda ya Kaskazini kuanzia saa 2.30 asubuhi na Jumatano tarehe 18/05/2022 kwa kanda ya Pwani kuanzia saa 2.30 asubuhi na kanda ya Kusini kuanzia saa 7.30 mchana kupitia mtandao wa Zoom/Webinar.
Malengo ya Warsha
Tarehe za kusajili ni kuanzia tarehe 13/05/2022 hadi tarehe 16/05/2022. Kiungo cha kusajili (Zoom/Webinar Link):
i. Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Dodoma, Singida, Tabora
Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Shinyanga and Simiyu):
https://thefoundation-or-tz.zoom.us/webinar/register/WN_GsUwXAeoS_OC3ewKUIYjNw
ii. Kanda ya Pwani (Dar es Salaam, Lindi, Morogoro, Mtwara, Pwani
Mjini Magharibi, Kaskazini Pemba, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba and Kusini Unguja):
https://thefoundation-or-tz.zoom.us/webinar/register/WN_Ad14pAcUQx-qh2TnXPHpTw
iii. Kanda ya Kusini (Iringa, Mbeya, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Songwe, Katavi and Kigoma):
https://thefoundation-or-tz.zoom.us/webinar/register/WN_VWmXuNbvQM6-5CwOHyTMlw