Kuhusu sisi

Foundation for Civil Society (FCS) ni shirika huru la Watanzania lisilo lenga kupata faida ambalo hutoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa Asasi za Kiraia (AZAKI) ili kuongeza ufanisi wao katika kuwezesha ushiriki wa wananchi kwenye michakato ya maendeleo. Shirika hili lilianzishwa na wadau wa maendeleo nchini Tanzania.

FCS ilianzishwa na kusajiliwa mwezi Septemba 2002 na kuanza kufanyakazi rasmi mwezi Januari 2003. Safari ya Foundation for Civil Society ilihusisha wadau wengi wa maendeleo ikiwemo Serikali na washirika wa maendeleo (DPs) ambao walikubaliana kuwa kuna upungufu wa rasilimali za umma za kusaidia Asasi za kiraia, na hivyo waliamua kutafuta njia ya kuweka mfumo mbadala wa kutoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa asasi za kiraia kote Tanzania, Bara na Zanzibar. Shirika hili linasimamiwa na Bodi huru.

FCS inawawezesha Wananchi kuwa chachu imara ya mabadiliko kwenye kuboresha utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania, kupambana na umasikini na kufikia maisha bora kwa wote. Hakika, shirika hili limekuwa kutoka wazo dogo lililobuniwa hadi kuwa taasisi kubwa yenye nguvu. Ndani ya miaka 15 ya kufanya shughuli zetu hapa nchini, tumekusanya zaidi ya Tshs bilioni 200 kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, na kuziwekeza kwenye kuziwezesha AZAKi zaidi ya 5,000 nchini kote kutekeleza miradi kadhaa ambayo inashughulikia changamoto nyingi za maendeleo ya jamii kwa wananchi wa mikoa yote ya Tanzania, Bara na Visiwani (Zanzibar). Tumewafikia Watanzania zaidi ya milioni 30 kwa muongo mmoja na nusu tuliofanyakazi. Na hivyo, hii imetufanya tuwe shirika la kutoa ruzuku lililowafikiwa watu wengi zaidi ngazi za jamii. Idadi ya AZAKi tulizoziwezesha na thamani ya rasilimali zetu zote tulizowekeza kuziimarisha AZAKI inatufanya kuwa taasisi kubwa ya kutoa ruzuku isiyolenga kupata faida katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Dira na malengo vimewezeshwa, na Watanzania wanaojituma wanafanikiwa kufikia haki ya uchumi wa kijamii na hali bora ya maisha ya watu.

Sisi ni nani

Foundation for Civil Society (FCS) ni asasi huru ya maendeleo nchini Tanzania isiyolenga kupata faida ambayo hutoa ruzuku na huduma za kujenga uwezo kwa Asasi za Kiraia za Tanzania.


Kwasasa ni moja ya Taasisi kubwa, na chanzo kikuu cha ufadhili kwa AZAKi za Kitanzania – kwahiyo, FCS inaziwezesha moja kwa moja AZAKi na wananchi kuwa chachu muhimu na mstari wa mbele kushawishi utawala wa kidemokrasia nchini Tanzania na maisha bora kwa watu wote. Kwahiyo, FCS ni mfadhili na mwezeshaji wa kati wa AZAKi nchini Tanzania na anayelenga kuwezesha ushiriki mzuri wa AZAKI kwenye jitihada za kupunguza umasikini kwa njia ambazo zinaambatana na juhudi za serikali na Washirika wa Maendeleo(DPs)kuelekea kupunguza umasikini kama ilivyopangwa kwenye miongozo mikuu ya maendeleo ya Tanzania: Dira ya Taifa ya Maedeleo ya 2025 na Mpango…

Soma Zaidi

Dira

Wananchi waliowezeshwa, wastahimilivu, wanaowajibika na wanapata haki za kiuchumi, kijamii na maisha bora.

Dhamira

Kuchangia maendeleo endelevu na jumuishi nchini Tanzania kwa kuimarisha uwezo na upatikanaji wa rasilimali. Tunafanya hivyo kupitia ushirikiano wa kimkakati na AZAKi, vikundi vya kijamii na wadau wengine wa maendeleo

Tunu za Msingi

Maadili ya msingi yanayoongoza FCS ni pamoja na: Usawa wa kijinsia & Ujumuishi, Unyenyekevu, Uwezo wa kukabiliana na mabadiliko na Wepesi wa kufikiri na Kutenda, Uadilifu na Uwajibikaji pamoja na Kujifunza na Umahiri

Utawala