Tunajenga na kuendeleza uwezo wa nani?
Kwa kuzingatia majukumu na wajibu wake wa kipekee wa kukuza AZAKI Tanzania, huduma za kujenga uwezo za FCS zimejikita kwenye kukuza uwezo wa watendaji na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni pamoja na:-
- Watu binafsi: Kama vile viongozi wa AZAKI, wafanyakazi wanaofanya kazi kwa kutembelea jamii, wanajamii, pamoja na wanawake na vijana, watunga sera na viongozi wengine wa serikali n.k. Tunatambua kuwa mabadiliko hutokana na athari za hatua anazochukua mtu mmoja mmoja na hatua za pamoja. Hata hivyo, mabadiliko kwenye ngazi ya mtu mmoja mmoja ni muhimu zaidi kwa maendeleo ya asasi na jamii. Kwa kawaida malengo ya kukuza uwezo katika ngazi hii yamelenga kutoa mafunzo yaliyojikita katika kukuza ujuzi wa wafanyakazi na wana-AZAKI.
- Asasi/Mashirika: FCS inatambua kuwa mahitaji mengi ya asasi ni zaidi ya ukosefu wa rasilimali na ujuzi. Kwahiyo, tunafanya mchakato wa kina wa ki-shirika wa kuongeza hamasa na kuchochea mabadiliko ya asasi. Mchakato huo unafanywa kwa njia ambayo umiliki wa mchakato wa mabadiliko umewekwa mikononi mwa asasi husika.
- Mtandao wa asasi, Harakati na Jumuiya: Msaada wa kujenga na kuendeleza wa uwezo kwenye ngazi hizi unatilia mkazo makundi fulani fulani ya asasi, kwahiyo kuna usawa na maslahi ya pamoja miongoni mwa sekta mbalimbali. Lengo ni kuimarisha uwezo sanjari na maeneo maalum yenye maslahi ya pamoja na uboreshaji wa makundi hayo. Mkazo mkubwa zaidi umejikita kwenye kukuza uwezo wa kimahusiano, kwa lengo la kuimarisha sauti ya pamoja na wasifu wa makundi hayo maalum ya wadau na watendaji wa kijamii.
Kujenga uwezo wa kisekta
Katika ngazi hii, unalenga sekta nzima ya asasi za kiraia badala ya asasi moja moja. Ujenzi wa wezo katika eneo hili unatazama mahitaji ya pamoja ya sekta nzima ya asasi za kiraia na jinsi ya kuimarisha sekta hii. Mkazo mkubwa unawekwa katika kubainisha malengo ya sekta hii na heshima na umuhimu wake kwa maendeleo
FCS inajengaje uwezo kwa taasisi?
Katika kujenga uwezo wa kisekta, FCS inatumia mbinu na staili mbalimbali za kujifunza zikiwemo kuwezesha taasisi kujitathimini, mafunzo ya ana kwa ana, kutoa msaada wa kitaaluma katika kuandaa sera na miongozo ya taasisi husika, warsha zinazohusisha wadau muhimu wa taasisi na ushauri elekezi, mabadiliko katika utawala na ukuaji wa taasisi, kubadilishana uzoefu kupitia majukwaa, semina na mikutano, safari za kujifunza kwa wadau wengine, usimamizi kwa vitendo na utoaji wa maelekezo kwa vitendo, tafiti na uchambuzi na upashanaji wa taarifa.