c Expand All C Collapse All

Ilitumwa Septemba 16, 2019

Zifuatazo ni aina tatu za ruzuku zinazotolewa na FCS: –

  1. Ruzuku ya Kimkakati: Hii ni ruzuku kubwa zaidi ambayo FCS inatoa kwa Mitandao ya Asasi za kiraia, Mashirika Mwamvuli ya Asasi za Kiraia yaliyo makini na yenye kufanyakazi kwa mafanikio na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi ngazi ya Kitaifa na zenye rekodi nzuri ya kusimamia fedha na kuleta matokeo yanayoonekana kote Tanzania. Mashirika ya aina hii yanapewa ruzuku kama “Viongozi wa Klasta” yaani, kwa mfano – kiongozi kwenye kundi la Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma au Ufuatiliaji wa Uwajibikaji Jamii; kiongozi kwenye kundi la Utetezi dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia na vitendo vibaya vya kimila nk. Mashirika haya yanapanga programu zao kwa namna ambayo wataweza kufanya kazi na AZAKi za kijamii zinazofanya kazi kwenye sekta na maudhui yao na kutumia mambo waliyojifunza kutoka ngazi ya jamii kushawishi utetezi kwa ngazi ya kitaifa, wakati huo huo wakitumia mambo waliyojifunza ngazi ya kitaifa kuyapeleka kusaidia kufanikisha miradi ngazi ya jamii.
  2. Ruzuku ya Kati: Aina hii ya ruzuku ndio imebeba sehemu kubwa ya kazi ya utoaji ruzuku ya FCS. Aina hii ya ruzuku inalenga mashirika ya kiwango cha kati ambayo yameonesha uwezo mubwa katika kusimamia mradi na matumizi ya fedha.
  3. Ruzuku ya Ubunifu: Ruzuku ya ubunifu imeyalenga mashirika ambayo yatatekeleza mikakati bunifu ya kuleta ufumbuzi na utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii kulingana na matokeo tarajiwa ya FCS. Dirisha hili pia linatoa fursa kwa asasi ndogo na mpya pamoja na zile changa ambazo zina mawazo bora ya kusaidia kuboresha changamoto za utawala maeneo yao. Pia inajumuisha mashirika ambayo yatapata ruzuku chini ya Tsh 50,000,000 / = na ambayo wanakusudia kutekeleza miradi nchini kote lakini kwa kufuata maudhui ya maeneo ya matokeo yaliyopangwa na FCS.
Category: Swahili

Ilitumwa Januari 14, 2020

Foundation inaweza tu kutoa ruzuku kwa mashirika ambayo yameanzishwa kwa malengo yasiyo kupata faida. Hata kama shughuli unayoombea ruzuku ni ya uhisani au msaada wa kiutu, hautastahili kupata ruzuku kama katiba yako haijasema wazi hali ya uhisani ambayo shirika lako limepanga kuitekeleza. Kama unafikiri shirika lako linaweza kuathiriwa na sharti hili, tafadhali pata ushauri kutoka FCS kabla ya kutuma maombi.

Foundation haitatoa ruzuku kwa mambo yafuatayo:

  • Gharama zisizotarajiwa (dharura). Matoleo/shukrani & ufadhiliwa wa masomo
  • Miradi au shughuli zilizo nje ya Tanzania.
  • Miradi au shughuli ambazo tayari zimekamilika
  • Miradi ambayo inatoa ruzuku kwa mashirika mengine.
  • Posho ya asante kwa wafanyakazi wa kuajiriwa
  • Shughuli za kuingizia kipato/mikopo midogo midogo
  • Soko la kipato / shughuli ndogo za fedha
  • Maombi kutoka kwa wataalamu wa kuchangisha fedha au Wataalamu-washauri wanaofanya kazi kwa niaba ya mashirika
  • Mtu mmoja mmoja
  • Vyama vya siasa.
  • Miradi inayotangaza dini fulani, kabila/kundi Fulani, rangi fulani au utamdanui fulani
  • Biashara za sekta binafsi (isipokuwa kama hazitoa faida binafsi)
  • Mashirika ambayo yana madeni makubwa.
  • Semina au Makongamano ya kujitegemea
  • Semina, isipokuwa kama ni sehemu ya shughuli zilizopangwa na zinahusiana na matokeo tarajiwa
  • Gharama zisizotarajiwa (dharura).
  • Utoaji wa huduma za kijamii
  • Maombi ya Ruzuku ya kimkakati ya kutekeleza miradi isiyoendana na mpango mkakati wa FCS.
Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

HAPANA, FCS haitoi ruzuku kwa Mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

HAPANA, FCS haitoi ruzuku kwa mtu mmoja mmoja.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

 FCS itatoa aina kuu mbili za matangazo ya wito wa kutuma maombi/maandiko mradi kama ilivyooneshwa hapa chini:

i) Tangazo la jumla la kutuma maombi: FCS itatoa angalau tangazo mmoja la kutaka waombaji wawasilishe maombi kama ilivyoainishwa kwenye mpango wa kila mwaka kulingana na matokeo ya maeneo muhimu ambayo ni utawala bora na Ustawi wa Jamii /Maendeleo ya Kiuchumi. Tangazo la jumla litatolewa mwezi Novemba kila mwaka au mwezi Januari wa mwaka unaofuatia au litatolewa kulingana na upatikanaji wa fedha na kwa kuzingatia maamuzi ya wakati huo ya menejimenti.

ii) Tangazo la kutuma Maombi maalum: Hili ni tangazo linalotolewa kwa lengo la kuwezesha utekelezaji kwenye masuala maalum au kutoa mwitikio wa haraka kwa masuala yanayoibuka yenye masilahi ya kitaifa kwenye maeneo ya utawala bora na Mahitaji ya maisha/Maendeleo ya Kiuchumi. Tangazo maalum pia litatolewa kwa lengo la kuwavutia waombaji wa ruzuku kwenye miradi maalum ambayo iko nje ya fedha za mfuko mkuu. Wakati mwingine pia na kwa kuzingatia mahitaji maalum yanayoweza kujitokeza, FCS inaweza kuwasiliana na asasi fulani ili kutatua masuala muhimu au kutekeleza kazi maalum. Namba za utambulisho wa Mradi zitaainishwa kwa kuzingatia dirisha la ruzuku na jina la wafadhili maalum wanaogharamia programu hiyo. Katika matangazo yote mawili, maombi ya Ruzuku hufanywa kupitia Fomu maalum iliyotolewa ambayo inapatikana kwa lugha zote mbili yaani katika Kiswahili au Kiingereza na hivyo, asasi inaweza kuomba kwa kutumia lugha mojawapo kati ya hizo mbili. Fomu hiyo ina maelekezo ya kina yanayofafanua kuhusu nini kinachohitajika. Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa kujaza moja kwa moja kwenye mtandao au kwa kujaza Fomu ya karatasi. Waombaji wa ruzuku watahimizwa zaidi kuwasilisha maombi kwa njia ya mtandao na kuhakikisha kuwa viambatisho vyote muhimu kulingana na maelekezo yaliyotolewa kwenye tangazo vimeambatanishwa. Hakutakuwa na tofauti ya aina ya viambatisho vilivyowasilishwa na waombaji kwa njia ya mtandao na wale watakaotumia Fomu za karatasi. FCS itatoa siku kati ya 21 hadi 30 kwa waombaji kuwasilisha maombi yao. Hata hivyo, kutokana na suala la ucheleweshaji wa fedha, menejimenti itaamua ni wakati gani muafaka wa waombaji wawasilishe maombi yao.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

Yafuatayo ni vitu vya lazima kukaguliwa.

  1. Sifa za mwombaji kulingana na vigezo na masharti ya FCS
  2. Fomu ya maombi iliyojazwa kikamilifu
  3. Katiba ya ASASI
  4. Hati ya Usajili wa ASASI
  5. Taarifa ya Benki

Asasi yoyote ambayo iko kwenye orodha ya asasi zilizowekewa vikwazo au haijaweza kuwasilisha nyaraka zote za lazima zilizoorodheshwa hapo juu itaondolewa kwenye hatua ya mchujo.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

Ziara za uchunguzi hakiki ni muhimu katika kutathmini athari na vihatarishi vilivyopo kabla ya FCS kuwekeza fedha na muda wake. Waombaji wote wapya ambao wamefuzu mchakato wa mchujo watafanyiwa uchunguzi hakiki (Isipokuwa wale watakaofaulu kupewa msamaha kama ilivyooneshwa kwenye ukurasa wa kudhibiti vihatarishi). Wakati wa Uchunguzi hakiki tume ya FCS, itafanya uchunguzi wa kufika na kuona kwa macho hali halisi ya waombaji wote wanaotarajiwa kufadhiliwa. Zoezi hili linalenga kuhakiki ukweli wa taarifa za wafadhiliwa watarajiwa, kuchunguza na kutathmini uwezo wa ndani wa asasi sambamba na mahusiano ya asasi na wadau wake, wanufaika na mamlaka za serikali za mitaa. Katika kutekeleza zoezi hili pamoja na masuala mengine, washauri watatumia dodoso la Uchunguzi hakiki litakalotolewa na FCS. Zoezi hilo litafanywa na kampuni ambayo itateuliwa kupitia mchakato wa zabuni wa kawaida. Matokeo ya zoezi la Uchunguzi hakiki yatawasilishwa kwenye kikao cha menejimenti na ripoti zitapelekwa Idara ya Fedha na Uendeshaji.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

Wapokea ruzuku wote waliopitishwa kutokana na kufuzu mapendekezo yao ya miradi watapitia Mafunzo maalum yaitwayo Simamia Ruzuku yako (MYG). Mafunzo haya hufanyika kabla ya kusainiwa mikataba. Kwahiyo, kuhudhuria mafunzo siyo hakikisho kwamba mradi utapewa ruzuku na FCS. Ikitokea kuna masuala tata yanaibuka kabla ya kusaini mkataba, ambayo yanaonekana kuathiri mafanikio ya matokeo ya mradi na malengo yake yaliyowekwa, mkataba unaweza kufutwa.

Mafunzo yanalenga kujenga uwezo wa wafadhiliwa (wapokea ruzuku) juu ya usimamizi wa ruzuku katika maeneo ya usimamizi wa fedha na ruzuku, ufuatiliaji na tathmini, kuandaa mipangokazi mzuri na kuweka mfumo wa uwekaji mzuri wa taarifa za fedha za mradi wao. Washiriki wa mafunzo haya watakuwa watekelezaji wakuu wa miradi. Kujifunza kutokana uzoefu wa mikakati iliyopita, mafunzo ya MYG yanahitaji juhudi nyingi katika suala la maandalizi, vifaa na usimamizi wa wafadhiliwa watarajiwa kwenye tukio la mafunzo. Kwahiyo, Kwa kipindi fulani FCS inaweza kumtafuta wakala wa fedha kusimamia fedha zinazohusiana na mafunzo ya MYG. Lakini utekelezaji wa MYG yenyewe unafanywa na wafanyakazi wa FCS, na kama kuna ulazima mkubwa Wanatafutwa Wataalam-Washauri wa nje kusaidia na kujenga uwezo wa wafadhiliwa wakati wa mafunzo ya MYG.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

Mafunzo ya MYG hufanyika kwa siku 5.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

FCS inachukulia ufuatiliaji na tathmini kama mchakato muhimu ambao unaweza kushirikishana uzoefu wa kujifunza, kuimarisha kufaa kwa program na ufanisi wake na kuhakikisha kuwa FCS na wafadhiliwa wake wanawajibika kufikia matokeo yaliyokusudiwa. Ziara za Ufuatiliaji na kutoa usaidizi ni sehemu muhimu ya mawasiliano na uhusiano wa ufuatiliaji kati ya Asasi/shirika na FCS. Ziara yoyote kwenye shirika inapaswa kusaidia kuwepo kwa mawasiliano ya wazi na chanya, vile vile usimamizi bora wa mradi na utoaji taarifa.

Lengo kuu la zoezi hili ni kuangalia mabadiliko yanayoweza kuonekana katika ngazi ya jamii kama matokeo ya moja kwa moja ya miradi ya FCS – kupitia ruzuku ya asasi za kiraia na mipango yake ya kujenga uwezo. Pia inaisaidia Foundation kuelewa vizuri kazi iliyofanyika kwenye jamii, kufuatilia maendeleo, kufuata sheria na masharti ya mkataba wa ruzuku, kujifunza na changamoto zilizopo.

Kila Mfadhiliwa(mpokea ruzuku) anatakiwa kutembelewa angalau mara moja kwa mwaka. Katika kila ziara, wafanyakazi wa FCS kabla ya kuondoka kwa mfadhiliwa wanajadili na wafanyakazi wa mfadhiliwa juu ya masuala yaliyobainika na kukubaliana namna ya kusonga mbele. Hii itafanyika kwa kujaza fomu ya kuondoka ya ziara ya kutoa usaidizi.

Kundi: M & E

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

Mifumo endelevu ya kudhibiti ipo ndani ya shirika ambayo ni pamoja na kujenga uwezo, uzoefu unaonesha miaka ya hivi karibuni kuna maboresho makubwa katika suala la kufuata sheria na taratibu hasa kwa AZAKi za kijamii ikiwa ni pamoja na AZAKi changa zinazochipukia. Wakati kuna vihatarishi vingi vinavyohusiana na kutoa ruzuku, hatari za usimamizi wa fedha ni kubwa zaidi kwasababu zinagharimu rasilimali za FCS.

Kwahiyo, zifuatazo ni taratibu za kawaida zinazopaswa kufuatwa wakati wa utekelezaji na baada ya ukaguzi wa mahesabu: –

  1. Kama hatua ya kuzuia, FCS itafanya mafunzo ya kukuza uwezo kwa wafadhiliwa ili kuinua kiwango chao cha kuelewa masuala mbalimbali muhimu kama:
    • Kuripoti shughuli zilizotekelezwa
    • Maana na umuhimu wa kuwa na mifumo imara ya udhibiti wa ndani
    • Mgawanyo wa kazi na majukumu
    • Utunzaji wa rekodi, kupanga nyaraka na mifumo ya kuhifadhi mafaili
    • Udhibiti wa kutoa idhini
    • Ulinganishsi wa taarifa za kibenki na usimamizi wa pesa
    • Kukagua hali ya kufuata sheria, taratibu na sera
  1. Mara kwa mara FCS itafanya ukaguzi wa kawaida na wa kushtukiza kwa wafadhiliwa ili kuhakikisha kama wanafuata sheria na taratibu.
  2. Pale ambapo nyaraka zinakosekana FCS itaomba Asasi mfadhiliwa alete nyaraka hizo ndani ya siku 30 baada ya ukaguzi kukamilika.
  3. Pale ambapo michakato ya manunuzi haikuoneshwa kwa uwazi, FCS itaomba nyaraka za ushahidi kama ankara, kumbukumbu za vikao vya manunuzi, kuendana na taratibu za kufuata zilizokubaliwa kwenye kumbukumbu za vikao na vitu vingine vinavyoonekana.
  4. Pale ambapo hakuna ushahidi wa kutosha wa matumizi yaliyofanywa, FCS haitayatambua matumizi yenye shaka na kuitaka asasi irudishe fedha FCS na hivyo kupunguza kiwango cha matumizi yaliyoripotiwa.

Kuhusu matukio ambapo udanganyifu unashukiwa, FCS itahitaji kiasi cha fedha kilichothibitishwa kurudishwa, na kuripoti tukio hili kwenye vyombo vya serikali kama Ofisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) au Polisi ambao wana mamlaka na wameaminiwa kisheria kushughulikia kesi za jinai.

Category: Swahili

Ilitumwa Februari 5, 2020

FCS inapokea taarifa za udanganyifu kuhusu Wafadhiliwa wake kupitia baruapepe:

whistleblower@thefoundation-tz.org

Category: Swahili