Uwezeshaji kwa watu wenye ulemavu

Tanzania, kama zilivyo nchi nyingine za kiafrika watu wenye ulemavu (WWU) ni miongoni mwa  watu wanaobaguliwa na kuishi katika mazingira magumu katika jamii zao. Kwa kuzingatia hilo, taasisi ya Foundation for civil Society (FCS) iliamua kusaidia juhudi za kupigania na kutetea haki za watu wenye ulemavu. Msukumo wa FCS upo katika kufanya ushawishi na utetezi ili serikali na wadau mbalimbali  watekeleze yaliyomo katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Watu wenye Ulemavu na Sheria ya Mwaka 2010 kuhusu Watu wenye Ulemavu Tanzania. Mkataba na shria hiyo ina lengo la kuleta mabadiliko chanya ya kimuundo na ufanyaji maamuzi ili kujumisha haki za WWU.

Wakati huo huo, jitihada za FCS kupiga vita mauaji ya watu wenye ualbino yana lengo la kutetea haki zao na kuhakikisha umma wanaelimishwa na kufahamu kuhusu hali ya ualbino.  

Mikoa ambayo FCS inawexesha utekelezaji wa miradi kwa ajili ya watu wenye ualbino ni ile ambayo ina historian a matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino hapa nchini.

Juhudu za kuwasaidia miradi inayolenga WWU ni katika kuunga mkono malengo Endelevu ya Maendeleo Namba 10 na 11 yanayohusu kupunguza ubaguzi baina ya nchi na kuyafanya makazi kuwa jumuishi, salama na endelevu. Kwa kuzingatia lengo la pili la matokeo ya Mpango Mkakati wa FCS wa mwaka 2016-2021 FCS imejizatiti katika kutoa changamoto katika maeneo ya kupanua demokrasia, haki na kufanya maamuzi ili WWU, vikundi vya kikabila na wanawake wapate haki ya kushiriki katika masuala yanayowahusu.

Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016-2018, jumla asasi za kiraia 18 zilipewa ruzuku na FCS ili kutekeleza miradi inayotetea haki za WWU na dhidi ya mauaji ya watu wenye ualbino. Asasi 8 zilipata ruzuku ili kutekeleza miradi kwa ajili ya WWU katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Simiyu, Geita,, Tabora na Shinyanga ambayo ina matukio mengi ya mauaji na ukataji viungo vya watu wenye ualbino.

Asasi 10 zilipewa ruzuku ili kutekeleza miradi kwa ajili ya WWU katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Dodoma, Kagera, Kigoma, Mwanza na Morogoro.

 

 

FCS inasaidia miradi ya aina gani?

FCS imeziwezesha asasi za kiraia zenye madhumuni ya kupunguza changamoto zinazowakabii WWU na kuhakikisha ulinzi na usalama kwa watu wenye ualbino, yakiwemo mapungufu ya kisera, utekelezaji na utoaji wa huduma. Shughuli zinazotekelezwa ni pamoja na:-

 • Kutoa mafunzo kuhusu Sheria Namba 9 kuhusu WWU ya mwaka 2010 na Mkataba wa Kimataifa wa mwaka.
 • Ushiriki wa vyombo vya habari (kama matangazo yenye ujumbe mfupi kwa njia ya radio na televisheni
 • Kutoa elimu kwa umma  kupitia nyenzo za mawasiliano kama vipeperushi
 • Kufanya utetezi na mikakati ya kuwahirikisha viongozi wa jamii, watu mashuhuri kama wabunge
 • Kampeni za uhamasishaji jamii

 

Viashiria

FCS imejikita katika kufuatilia na kuona

 • Idadi ya taarifa au visa vinavyoonesha hatua mbalimbali zilichukuliwa na jamii, viongozi ili kukabiliana na mila zilizopitwa na wakati.
 • Asilimia ya asasi za kiraia zinaotoa taarifa kuwa serikali imejizatiti na kuchukua hatua stahiki  kukidhi mahitaji ya makundi ya watu wanaoishi katika mazingira magumu

Matokeo na viashiria kwa miradi inayowalenga WWU

 • Idadi ya watu waliofikiwa (Wanawake na Wanaume)
 • Idadi ya watu walioingia katika vyombo vya kufanya maamuzi
 • Idadi na aina ya mapendekezo yaliyofanywa na wadau wenye dhamana ya kulinda haki za WWU
 • Idadi ya huduma na watu waliopata kuhudumiwa na bajeti iliyopo kuhusu ulinzi na usalama wa WWU na sharia au sera zilizofanyiwa marekebisho
 • Kuwepo kwa sharia na seria ndogo ndogo kuhusu haki za WWU

 

Matokeo ya miradi hadi mwaka 2017

 • Hadi mwaka 2016-2017 jumla ya WWU wapatao 70,795 (wakiwemo wanawake 35,920, wanaume 34,875) wamefikiwa na miradi ya asasi zinazopewa ruzuku na FCS na wengine 70,459 (Ke 33,951, Me: 36,508) kupitia asasi za watu wenye ulemavu.
 • Mabadiliko ya miundo mbinu katika majengo ya sekta za elimu, afya, mabenki na maeneo ya umma kuwasaidia WWU katika wilaya za Kibaha, Korogwe, Biharamulo na Kwimba.
 • Serikali katika Halmashauri ya wilaya ya Kwimba ilianzisha kitengo au darasa kuhusu watu wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi ya Budishi
 • Bajeti za serikali kadhaa za mikoa zimeweka zimejumuisha shughuli zinazolenga WWU
 • Ongezeko la uelewa na ufahamu kuhusu haki za WWU uliosaidia watendaji katika mkoa wa Mara kuunda Kamati za WWU mpaka ngazi ya wilaya
 • Serikali za mitaa zimejizatiti katika kutetea haki za WWU
 • Kuwajumuisha WWU katika mchakato wa kupanga, kufanya maamuzi na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
 • Kutoa elimu kuhusu haki za WWU kwenye matukio kama Siku ya WWU
 • Uundwaji wa vikundi vya ulinzi wakati wa usiku kulinda maisha ya watu wenye ualbino
 • Kuwatambua WWU waliofichwa na familia zao kwa sababu mbalimbali kama usalama, Imani potofu na unyanyapaa

Washirika wa FCS kwa ajili ya Miradi kwa WWU

Hadi mwaka huu, FCS imeshatoa ruzuku zinazofikia Shilingi milioni 600 kuziwezesha asasi kutekeleza miradi inayowalenga Watu wenye |Ulemavu kama ifuatavyo

Na. Taasisi Mkoa/Wilaya
1. Tanzania League of the Blind Dar es Salaam
2 Tanzania League of the Blind Dodoma
3. Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania Kigoma
4. Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania Dodoma
5. Umoja wa Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Pwani Pwani
6. Chama cha Wasioona Kilosa Morogoro
7. Tanzania Association of the Deaf Dar es Salaam
8. Registered Trustees of the RC Church-Ngara Kagera
9. Tanzania League of the Blind Kwimba Mwanza
10. Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania-HQ Dar es Salaam

 

Washirika wanaotekeleza miradi kwa Watu Wenye Ualbino

Kwa sasa, FCS imetoa ruzuku zenye thamani ya Shilingi milioni 500 kwa asasi zinazotekeleza miradi kwa ajili ya Watu wenye Ualbino kama ifuatavyo:-

Na. Asasi Mkoa/Wilaya
1 Sumbawanga Association of NGOs (SUMANGO) Rukwa
2. Grace Community Development & Education Rukwa
3. Mass Media Bariadi Simiyu
4. Catholic Archdiocese of Tabora Tabora
5. Newlight Children Organization-NELICO Geita
6. Chama cha Albino Tanzania Bukombe Simiyu
7. Radio Faraja Shinyanga
8. Nabroho Society for the Aged Simiyu

 

Kupambana na mila potofu na hatarishi

Katika kukabiliana na mila na desturi hatarishi, FCS imejikita zaidi katika kupamba na Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, watoto kuolewa katika umri mdogo na aina nyingine za ukatili na unyanyasaji. Licha ya kuwepo sheria zinazozuia na kutoa adhabu dhidi ya uendelezaji wa mila na desturi hatarishi bado mila hizo zinaendelea kuwapo kutokana Imani za kishirkina na mila. Ukatili wa kijinsia ni kitendo ukiukwaji wa wa haki za binadamu. Hali hii imezikumba sehemu mbalimbali za nchi hii. Hali kama hii pia inahusu ukatili wa kingono na ukeketaji ambapo waathirika hukumbwa na matatizo mengi ya kiafya wakati wa kujifungua kama utokwaji wa damu nyingi wakati wa kujifungua na hata kifo.

Mkoa wa Mara ndio wenye kiwango kikubwa cha visa vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ukeketaji unaowahusisha wasichana wadogo wasiozidi miaka 15. Mikoa mingine yenye kiwango kikubwa cha visa vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma na Simiyu.

Sababu kubwa inayoifanya FCS kuunga mkono juhudi za asasi za kiraia kupambana na mila potofu ni kwa vile desturi hizo zinakiuka haki za binadamu hususan wanawake na watoto. Kimsingi, miradi hii inayotekelezwa na FCS kwa ruzuku ya FCS ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuondoa ukiukwaji wa haki kwa misingi ya jinsia ndani ya jamii. Pia asasi zinasaidia kuihamasisha juhudu za jamii na serikali za mitaa katika kukabiliana na ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto kwa ajili ya kuwapatia wananchi maendeleo endelevu.

FCS inavyofanya kazi

Jitihada mbalimbali za miradi inayofadhiliwa na FCS ina lengo la kubadili mtazamo wa wanufaika na miradi hiyo kuhusu mila na desturi potofu. Mkazo pia unawekwa katika kuwawezesha waathirika, asasi pamoja na wananchi kwa ujumla waweze kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na wa kingono kwenye vyombo mbalimbali zinavohusika na sheria na kuwalinda wananchi kwa ajili ya hatua zaidi lakini pia kuimarisha mifumo na miundo ya kitaasisi ili iweze kubaini na kushughulikia kadhia hii.

FCS inafanya kazi na asasi za mashinani kwa kuwalenga wanufaika lakini pia inafanya na halmashauri za wilaya. Aadhi ya mikakati na mbinu zinazotumiwa katika kukabiliana na tatizo hili ni pamoja na:

 • Uhamasishaji jamii kupitia mikutano, maonesho ya njiani na kwenye maeneo ya watu wengi ili kutoa elimu na ufahamu zaidi kuhusu athari za ukatili wa kijinsia, ukeketaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia.
 • Kuwapa mafunzo viongozi, wataalam na viongozi wa mila na wa dini na wale wanaoendeleza mapambano dhidi ya mila potofu katika maeneo yao
 • Kujenga mtandano wa wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ukiwajumuisha waelimisha rika, watu wa mfano wa kuigwa katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia ili waweze kutoa taarifa na kufuatilia matukio mbalimbali
 • Kutoa elimu na hamasa kwa jamii kupitia vyombo vya habari kama vipeperushi, vipindi vya redio, majarida na machapisho mbalimbali, michezo ya kuigiza, michezo na matukio ya kijamii
 • Uundwaji na uendelezaji wa majukwaa ya kupinga ukatili wa kijinsia, ukeketaji kwa njia ya vikundi vya watoto kama mabalozi wa kutetea haki zao

Matokeo tarajiwa

 1. Uundwaji wa majukwaa ya kijamii ya kuinga ukatili wa kijinsia, ufuatiliaji na kutoa taarifa za matukio kwa taasisi husika
 2. Kuweka mkakati unaojumuisha sekta mbalimbali ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukeketaji
 3. Kuweka sheria ndogo ndogo ili kuwalinda wanawake na watoto

Wadau wetu

Kwa sasa FCS imetia ruzuku kwa asasi 31 zinazotekeleza miradi ya kukabiliana na mila potofu ikiwemo ukatili wa kijinsia, ukeketaji na uozaji watoto katika umri mdogo katika mikoa mitano ambayo ina idaid kubwa ya visa na matukio ya mila na tabia hizi hatarishi. Mikoa hiyo ni Mara, Singida, Dodoma, Kiimanjaro, Shinyanga na Manyara. Jumla ya Shilingi bilioni 1.9 zimetolewa na FCS kama ruzuku kwa ajili ya asasi zinazotekeleza miradi hii.