UTOAJI WA RUZUKU

Taasisi ya FCS inatoa ruzuku kwa asasi za kiraia ili ziweze kuinua maisha ya watu hususan wale wanaoishi kwenye mazingira magumu na pembezoni ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza umaskini. Ni taasisi mahiri inayotoa ruzuku.

 

Maombi ya kupatiwa ruzuku hufanyika tu baada ya FCS kutangaza wito wa kutuma maombi ya ruzuku kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari, mitandao yake ya kijamii  na tovuti yake.

 

Aina za ruzuku zitolewazo na FCS:

Ruzuku za kimkakati

Kiwango cha ruzuku hizi zina thamani ya Shilingi million 750 katika kipindi cha miaka mitatu ambapo kila mwaka hutolewa kiasi cha shilingi milioni 250.

 

Ruzuku ya kati

Ruzuku hizi zina thamani ya Shilingi milioni 360 ambazo zitatumika katika kipindi cha miaka mitatu kwa wastani wa shilingi milioni 120 kwa mwaka

 

Ruzuku ya ubunifu

Ruzuku hii ni kwa ajili ya asasi ambazo zinatumia ubunifu wao katika kutatua matatizo yanayowakabili wananchi. Miradi inayopatiwa ruzuku hii  ni ile inayotekelezeka miradi katika kipindi cha mwaka mmoja ambapo asasi inaweza kuomba kiasi cha shilingi milioni 20 hadi milioni 50.