Ufuatiliaji wa uwajibikaji kwa jamii

Msukumo mkubwa wa FCS katika mkkakati huu ni uhakikisha kuwa serikali za mitaa zinatoa huduma bora kwa wananchi. Msukumo huu utafikiwa kwa kuzitumia asasi zinazotekeleza miradi inayosisitiza usimamizi wa rasilimali za umm na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma na ushiriki wa wananchi katika kupanga, kuandaa bajeti na sera. Katika Mpango Mkakati wa sasa sekta muhimu zinazotiliwa mkazo ni za maji, elimu na kilimo.

Mikakati inayotumika kufikia malengo yaliyokusudiwa katika mkakati huu ni kwa kutumua nyenzo mbalimbali zikiwemo:

  • Ufuatiliaji wa Matumizi ya fedha za Umma
  • Ufutiliaji wa Uwajibikaji kwa Umma
  • Njia shirikishi zinazowezesha wananchi kushiriki katika kupanga na kuandaa bajeti

Inatarajiwa kuwa ushirikiano wa karibu kati ya asasi za kiraia, wananchi na wadau wengine utazisukuma serikali za mitaa kufanya shughuli zake kwa uwazi na uwajibikaji na kuheshimu misingi ya utawala wa sheria na kanuni zilizowekwa. Pia kuhakikisha kwamba wananchi wameshiriki kikamilifu katika kupanga mipango, kuandaa bajeti na kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi ili kuwezesha upatikanaji wa huduma stahiki kwa jamii.

Lengo la FCS katika mkakati huu ni kuona kwamba serikali za mitaa zinakuwa madhubuti ili kuweza kutoa huduma bora za jamii kwa wananchi katika maeneo yao. Shughuli za mkakati huu zinahakikisha kuwa wananchi wanashiriki na kushikishwa kikamilifu katika kufuatilia jinsi mamlaka husika zinavyotumia rasilimali na fedha zilizopo. Inaeleweka kwamba utendaji mzuri wa serikali za mitaa unaleta Imani zaidi kwa wananchi na kuongeza morali yao katika kutekeleza shughuli za maendeleo.

FCS inavyofanya kazi

FCS inafanya kazi na asasi ambazo zinadhihirisha jinsi zinavyochangia kuzifanya serikali za mitaa kuwajibika na hivyo kuzifanya serikali hizo kutoa huduma bora kwa wananchi wake. Kila asasi impagwa katika sekta husika na inashirikiana na wadau wa pande zote ikiwemo mitandao na watu binafsi. Njia hii inawezesha ujenzi wa asasi kutoka ngazi ya chini hadi kitaifa katika kukabiliana na changamoto za utawala bora na uwajibikaji. Mafunzo yatokanayo na utekelezaji wa miradi hiyo na mifano mizuri ya kuigwa kutoka kikundi cha sekta moja hutolewa kama funzo kwa kikundi cha sekta katika asasi za ngazi ya wulaya, mkoa hadi taifa.

Wadau wetu

Mpaka sasa FCS imekwisha toa ruzuku ya jumla ya Shilingi bilioni 1.4 kwa asasi 29 zinazotekeleza miradi yao kwa mwaka 2016-2017. Kiasi cha shilingi bilioni 3 zimetolewa kwa asasi 57 kwa shughuli hizo hizo kwa mwaka wa fedha wa 2017-2018

Matokeo tarajiwa

FCS inatarajia kuona matokeo mabadiliko katika taasisi za serikali zinazotokana na msukumo wa ufuatiliaji wa uwajibikaji na hivyo kuzifanya serikali za mitaa kutoa huduma bora kwa wananchi. Matokeo ya sasa ni pamoja na:

  • Asasi 29 zilipata ruzuku ya miradi ya ufuatiliaji uwajibikaji na ufuatiliaji wa fedha za umma katika mikoa 12 ya Mwanza, Morogoro, Singida, Kigoma, geita, kagera, Manyara, Tanga na Kilimanjaro
  • Miradi hiyo iliwafikia wananchi 68,713 (Ke 29,627, Me: 39,086)
  • Ongezeko la ufahamu kuhusu uwajibikaji na umuhimu wa kufanya shughuli kwa uwazi miongoni mwa viongozi na wananchi
  • Jumla ya kamati 42 za Ufuatiliaji wa Matumizi ya Umma ziliundwa kupitia miradi 63 katika sekta ya elimu katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Manyara, Tanga na Morogoro. Kuna ongezeko la uwajibikaji na uwazi ¬†katika mapato na matumizi kutokana na miradi hiyo

Mwaka 2017, FCS ilitoa ruzuku kwa asasi 57 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ufuatiliaji matumizi ya fedha za umma na uwajibikaji katika sekta za elimu, maji na kilimo iliyohusisha upangaji mipango na bajeti na ushiriki wa wananchi.  Asasi 3 zilipewa ruzuku ili kutekeleza mradi wa ushirkishaji wanannchi katika uandaaji wa sera ngazi ya taifa. Miradi hii inatekelezwa katika mikoa ya Kigoma,Kagera, Mwanza, Singida, Lindi, Mtwara, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Ruvuma na Unguja.