Kupambana na mila potofu na hatarishi

Katika kukabiliana na mila na desturi hatarishi, FCS imejikita zaidi katika kupamba na Ukatili wa Kijinsia, Ukeketaji, watoto kuolewa katika umri mdogo na aina nyingine za ukatili na unyanyasaji. Licha ya kuwepo sheria zinazozuia na kutoa adhabu dhidi ya uendelezaji wa mila na desturi hatarishi bado mila hizo zinaendelea kuwapo kutokana Imani za kishirkina na mila. Ukatili wa kijinsia ni kitendo ukiukwaji wa wa haki za binadamu. Hali hii imezikumba sehemu mbalimbali za nchi hii. Hali kama hii pia inahusu ukatili wa kingono na ukeketaji ambapo waathirika hukumbwa na matatizo mengi ya kiafya wakati wa kujifungua kama utokwaji wa damu nyingi wakati wa kujifungua na hata kifo.

Mkoa wa Mara ndio wenye kiwango kikubwa cha visa vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ukeketaji unaowahusisha wasichana wadogo wasiozidi miaka 15. Mikoa mingine yenye kiwango kikubwa cha visa vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma na Simiyu.

Sababu kubwa inayoifanya FCS kuunga mkono juhudi za asasi za kiraia kupambana na mila potofu ni kwa vile desturi hizo zinakiuka haki za binadamu hususan wanawake na watoto. Kimsingi, miradi hii inayotekelezwa na FCS kwa ruzuku ya FCS ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuondoa ukiukwaji wa haki kwa misingi ya jinsia ndani ya jamii. Pia asasi zinasaidia kuihamasisha juhudu za jamii na serikali za mitaa katika kukabiliana na ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto kwa ajili ya kuwapatia wananchi maendeleo endelevu.

FCS inavyofanya kazi

Jitihada mbalimbali za miradi inayofadhiliwa na FCS ina lengo la kubadili mtazamo wa wanufaika na miradi hiyo kuhusu mila na desturi potofu. Mkazo pia unawekwa katika kuwawezesha waathirika, asasi pamoja na wananchi kwa ujumla waweze kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na wa kingono kwenye vyombo mbalimbali zinavohusika na sheria na kuwalinda wananchi kwa ajili ya hatua zaidi lakini pia kuimarisha mifumo na miundo ya kitaasisi ili iweze kubaini na kushughulikia kadhia hii.

FCS inafanya kazi na asasi za mashinani kwa kuwalenga wanufaika lakini pia inafanya na halmashauri za wilaya. Aadhi ya mikakati na mbinu zinazotumiwa katika kukabiliana na tatizo hili ni pamoja na:

  • Uhamasishaji jamii kupitia mikutano, maonesho ya njiani na kwenye maeneo ya watu wengi ili kutoa elimu na ufahamu zaidi kuhusu athari za ukatili wa kijinsia, ukeketaji na aina nyingine za ukatili wa kijinsia.
  • Kuwapa mafunzo viongozi, wataalam na viongozi wa mila na wa dini na wale wanaoendeleza mapambano dhidi ya mila potofu katika maeneo yao
  • Kujenga mtandano wa wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia ukiwajumuisha waelimisha rika, watu wa mfano wa kuigwa katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia ili waweze kutoa taarifa na kufuatilia matukio mbalimbali
  • Kutoa elimu na hamasa kwa jamii kupitia vyombo vya habari kama vipeperushi, vipindi vya redio, majarida na machapisho mbalimbali, michezo ya kuigiza, michezo na matukio ya kijamii
  • Uundwaji na uendelezaji wa majukwaa ya kupinga ukatili wa kijinsia, ukeketaji kwa njia ya vikundi vya watoto kama mabalozi wa kutetea haki zao

Matokeo tarajiwa

  1. Uundwaji wa majukwaa ya kijamii ya kuinga ukatili wa kijinsia, ufuatiliaji na kutoa taarifa za matukio kwa taasisi husika
  2. Kuweka mkakati unaojumuisha sekta mbalimbali ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia na ukeketaji
  3. Kuweka sheria ndogo ndogo ili kuwalinda wanawake na watoto

Wadau wetu

Kwa sasa FCS imetia ruzuku kwa asasi 31 zinazotekeleza miradi ya kukabiliana na mila potofu ikiwemo ukatili wa kijinsia, ukeketaji na uozaji watoto katika umri mdogo katika mikoa mitano ambayo ina idaid kubwa ya visa na matukio ya mila na tabia hizi hatarishi. Mikoa hiyo ni Mara, Singida, Dodoma, Kiimanjaro, Shinyanga na Manyara. Jumla ya Shilingi bilioni 1.9 zimetolewa na FCS kama ruzuku kwa ajili ya asasi zinazotekeleza miradi hii.