Kujenga amani na usimamizi wa migogoro

Madhumuni ya Mkakati huu wa Kuimarisha Amani na Usimamizi wa Migogoro ni katika juhudi za kutafuta amani kwa kujenga mahusiano mazuri ndani ya makundi mbalimbali ya watu nchini Tanzania. Mkakati huu unalenga kuimarisha na kujenga uwezo wa kuendesha mijadala na mazungumzo ya jinsi ya kutanzua migogoro baina ya raia na hivyo kuchangia uwepo wa amani na mshikamano katika tasnia ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Katika Mpango Mkakati wa mwaka 2016-2020, Taasisi ya FCS imejumuisha mkakati huu kama njia ya kuimarisha amani na kusimamia utatuzi wa migogoro kama sehemu muhimu ya mkakati wa Utawala Bora. Mkakati huu unaongeza mwelekeo mpya  wa majadiliano na utatuzi wa migogoro kati ya raia na serikali hususan katika maeneo ya majadiliano kuhusu migawanyiko ya kisiasa hasa katika migogoro ya ardhi. Katika uimarishaji wa amani mkazo mkubwa unawekwa kwenye majadiliano ya kutanzua migongano baina ya raia na raia au raia na serikali.

Kwa nini kutilia mkazo uimarishaji amani na usimamizi katika kutatua migogoro?

Uchambuzi wa hivi karibuni kuhusu uimarishaji amani na utatuzi wa migogoro unaleta taswira kuwa kuna viashiria vya kuvurugika kwa amani katika jamii ya watanzania inayohitaji kudhibitiwa mapema licha ya baadhi ya watu kuona kama ni dhambi kukubali kuwa kuna viashiria vya kutoelewana.

Hali halisi ni kwamba migogoro na tofauti imekuwa sehemu ya mijadala mikali ndani ya vyombo kama Bunge. Utatuzi wa migogoro na desturi ya kuzungumza inatoa funzo kuhusu njia za kufanya ili kuepusha mikinzano ili kufikia muafaka na makubaliano. Mtazamo huu potofu wa kuogopa na kukubali uwepo wa migogoro katika jamii umeondoa utamaduni uliozoeleka wa kufanya majadiliano na mazungumzo kama njia ya kufikia maafikiano na kuondoa migogoro.        

Vipaumbele vya mpango huu

  • Juhudi za kufanya mazungumzo ili kuondoa sintofahamu za kisiasa
  • Majadiliano na utatuzi wa migogoro itokanayo na ardhi
  • Migongano yenye misingi ya udini

Wanufaika wa miradi

Ili utatuzi wa migogoro kwa njia ya majadiliano uweze kufanikiwa, ni muhimu kuyashirikisha makundi mbalimbali. Mkakati huu utategemea na aina ya migogoro na uchambuzi wa jinsi jamii ilivyojikita katika na utambuzi wa wadau muhimu  katika kufanya maamuzikuhusu lini, kwa vipi, na kwa nini majadiliano yanaweza kuanzishwa (kwa mfano nani anakaa meza ya majadiliano, jambo ambalo linaweza kupingwa wakati wa mazungumzo ya kuleta muafaka baina ya vikundi. Wadau muhimu kwa majadiliano wanaweza kuwa wawakilishi wa serikali, wawakilishi wa vyama vya siasa, taasisi, viongozi wa mila, wa dini na asasi za kisiasa.

Mkakati huu pia unachagiza umuhimu wa kuyahusisha makundi ya wanawake na vijana  kama wadau muhimu na pia wadau muhimu wa kuanza mazungumzo katika jamii.

Matazamio ya miradi

  • Kuimarika kwa juhudi za muda mfui na muda mrefu za kuleta majadiliano na utatuzi wa migogoro
  • Kuundwa na kuimarishwa kwa majukwaa ya muda mfupi na muda wa kati kwa miundo na mifumo ya mazungumzo
  • Kuongezeka kw auelewa kuhusu sababu za migogoro kunakotokana na tafiti na uchambuzi  wa migogoro na njia za utatuzi na mrejesho wake

 

Jitihada za majadiliano na utatuzi wa migogoro

Jitihada hizi zinalenga katika kuunga mkono njia mbalimbali za kushughulikia kutoelewana, mizozo na mifarakano. Mfano halizi ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuuwa mwaka 2015 juhudi mbalimbali zilifanyika na vikundi mbalimbali kuwaleta wanasiasa wanaopingana ili kupunguza jazba na uwezekano wa kutokea mlipo uliofuatia kutoelewana wakati wa kampeni za uchaguzi huo na kwenye majimbo ili kupunguza uwezekano wa kutokea vurugu.

Msaada unaweza kuwa wa juhudi za muda mfupi au wa kati kwa asasi za kiraia zinazoweza kutatua mgogoro au kuzileta pamoja pande zinazokinzana kwenye meza ya majadiliano.  

Majukwaa ya majadiliano

Hapa mkazo unawekwa kwenye uundaji wa mifumo na miundo itakayowezesha kutatua migogoro na kuleta amani. Kwa mfano, Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimeanzisha majukwaa ya majadiiano katika wilaya 9. Majukwaa haya ni matunda ya mafunzo yaliyotolewa kwa wadau muhimu katika kupunguza sintofahamu baina ya wagombea wa zamani na wapya katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi. Awali, asasi z akiraia zilifanikiwa kuanzisha kamati za amani na majadiliano katika ngazi ya jamii kushughulikia migogoro ya ardhi. Majukwaa ya majadiliano ya lengo la kuzileta pamoja pande zinazogombana na zenye mgogoro ili kujadiliana jinsi ya kutanzua na kumaliza kabisa mgogoro husika.

Ufahamu kuhusu chambuzi za migogoro na utatuzi wake

Msisitizo hapa ni katika umuhimu wa kuwepo kwa taarifa, uchambuzi kuhusu migogoro na ufumbuzi wake hapa nchini. Uwezo uliopo katika taasisi za utafiti, elimu ya juu na taasisi zenye haki ya kutafiti, kuchambua na kuchapisha matokeo ya migogoro na ufumbuzi wake na kutoa elimu kuhusu utatuzi wa migogoro kupitia mafunzo ya sayansi ya siasa, mafunzo ya kidiplomasia, au mahusiano ya tamaduni mbalimbali yanaweza kuimarishwa kwa kujengewa uwezo. Tafiti zinaweza kutazama uzoefu kaitka kushughulikia migogoro ya kimataifa lakini pia kuchunguza na kupata mifano mbalimbali iliyopo Tanzaniakuhusu mazungumzo na jitiahda za utatuzi wa migogoro. Utoaji wa elimu kuhusu utatuzi wa migogoro katika shule unaweza ia kuwa sehemu ya mkakati huu.

Kwa sasa hakuna sera maalum ndani ya serikali inayoweza kusaidia juhudi za kufanya utetezi na kuzengea. Zipo jitihada zilizoanza kuhusu kujenga uwezo wa Mfumo wa Kutoa Tahadhari na Matokeo ya Awali ya kuchambua taarifa kuhusu viashiria vya migogoro ili kusaidia kuweka mfumo imara wa kudhibiti mgogoro kamili kutokea ukiongozwa na Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia na Kutoa Kuadhibu Makosa ya Mauaji ya Kimbari, Makosa Dhidi ya Binadamu wakati wa vita na aima mbalimbali za ubaguzi wakati wa migogoro. Kamati hii iliundwa mwaka 2012 chini ya Kamati ya Kimataifa ya Maziwa Makuu  ya Kuzuia, Kutoa Adhabu ya Makosa ya Kimbari, Makosa ya kivita dhidi ya binadamu na Aina Mbalimbali za Ubaguzi. Asasi za kiraia zinaweza kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo ya kimataifa (EWER).

Wadau na ruzuku

Hadi sasa, FCS imekwisha toa ruzuku inayofukia Shilingi milioni 690 kwa asasi 10 zinazotekeleza miradi katika eneo hili la kimkakati. Asasi hizo ni pamoja na mbili za kimkakati, asasi mbili zinazotekeleza mradi wa muda wa kati na sita zinazotekeleza mradi wa ubunifu.