Haki ya wanawake kumiliki ardhi

FCS inawasaidia wanawake kupata haki ya kumiliki ardhi

Mkakati huu una lengo la kutoa changamoto ya kisera sera na sheria ili ziweze kutoa matokeo yatakayowanufaisha watu maskini na wanaobaguliwa hasa wanawake. Licha ya ardhi kuwa ndiyo  rasilimali kubwa kwa wanawake hapa Tanzania na licha ya kuwepo kwa Sheria Namba 4 na 5 ya Ardhi ya mwaka 1999 na marejeo ya sheria hiyo ya mwaka 2002 iliyotoa nafasi kwa wanawake kumiliki ardhi, bado wanawake wengi hawapati haki stahiki ya kuwa na ardhi. Pia kwa mkakati huu, FCS inachangia utekelezwaji wa Lengo la Maendeleo Endelevu namba 5 linalolenga kuwepo kwa usawa wa kijinsia na kuwapa uwezo wanawake wote na wasichana kupitia miradi inayotetea haki zao za kumiliki ardhi na hivyo kuwawezesha wanawake kuwa na fursa sawa za kimaendeleo na sauti katika umiliki wa ardhi. Mbali na masuala ya ardhi, mkakati huu pia unahusu haki za wanawake katika masuala ya kifedha, mali asili na umiliki wa ardhi kwa mujibu wa sheria za nchi. Kwa upande mwingine, mkakati huu pia una lengo la kupiga vita mila na desturi zinazowafanya wanawake wachukue nafasi ya pili kwa umuhimu katika masuala ya ardhi nyuma ya wanaume na kutotoa fursa sawa baina ya jinsi hizi mbili katika masuala ya umiliki wa rasilimali ikiwemo ardhi.

Matokeo tarajiwa:

  1. Kuwepo na utawala wa haki nchini Tanzania unaotokana na juhudi za asasi za kiraia zilizopewa ruzuku na FCS
  2. Kuongezeka kwa idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi

Viashiria vya matokeo

  1. Idadi ya watu waliofikiwa na elimu na uhamasishaji uliofanywa na asasi (idadi katika wanaume na wanawake)
  2. Idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi, ikiwemo wale wenye hati za kumiliki ardhi, wale waliorejeshewa ardhi na idadi ya wanawake walioshinda mashauri kuhusu madai ya ardhi
  3. Idadi ya migogoro ya ardhi iliyotatuliwa
  4. Idadi ya maamuzi yaliyofanywa na kuwatangaza wanawake kuwa washindi katika mashauri

Mbinu za utekelezaji

Dhana ya Utendaji (Theory of Action) ya FCS inatumia njia ya kuziweka asasi za kiraia kwenye vikundi mahsusi yanayowezeshwa na kada ya kitaalam inayoundwa na asasi za kimkakati za kitaifa zenye jukumu la kusimamisa utekelezaji wa mradi ya kisekta inayofadhiliwa FCS. Majukumu mengine ya asasi za kimkakati za kitaifa katika Dhana hii ya Utendaji ya FCS ni kufanya kazi na asasi za kati na zenye ubunifu katika sekta zinazohusika. Njia hii inasaidia asasi kujifunza kwa asasi nyingine zinazotekeleza miradi ya sekta zinazofanana na kuongeza ushiriki. Viongozi wa asasi za kitaifa huwa na kazi ya kuzisaidia asasi change na za ngazi ya chini kuongeza utendaji wake sambamba na viongozi hao kujifunza na kukusanya ushahidi kuhusu miradi mbalimbali na kuutumia katika kufanya utetezi wa masuala ya kisekta katika ngazi ya taifa.

Wadau wa FCS na ruzuku iliyotolewa

Kuanzia mwaka 2018, FCS imekwisha toa ruzuku yenye thamani ya Shilingi 900 kwa asasi 12 zinazotekeleza miradi inayolenga kuwapatia wanawake hazi zao katika masuala ya umiliki ardhi. Miongoni mwa asasi hizi moja ni ya kimkakati inayotekeleza mradi wa kuratibu shughuli za utetezi wa haki, kujifunza na kubadilishana uzoefu katika mikoa yote ya Tanzania.

Wadau

Na. Jina la asasi Aina ya ruzuku Kiasi (Shilingi) Mkoa
1. Utawala Bora, na Shughuli za Kujikimu (GGLIST) Ubunifu 40,800,000/- Morogoro
2 Chalinze Community Dev. Centre (CHACODE) Ubunifu 40,800,000/- Pwani
3. Mtandao wa Vikoba Ubunifu 45,800,000/- Singida
4. Chama cha Maendeleo ya Wanawake, Sayansi na Teknolojia (WODSTA) Ruzuku ya kati 70,800,000/- Arusha
5. Community Economic Development and Social Transformation (CEDESOTA) Ruzuku ya kati 70,800,000/- Arusha
6. Ujamaa Community Resource Team (UCRT) Ruzuku ya kati 120,100,000/- Manyara
7. Tanzania Womeen Lawyers Association (TAWLA) Ruzuku ya kati 70,800,000/- Arusha
8. Iringa Civil Society Organizations (ICISO) Ruzuku ya kati 60,800,000/- Iringa
9. Tanzania Rural Women and Children Development (TARWOC) Ruzuku ya kati 60,800,000/- Iringa
10. Women and Poverty Alleviation Tanzania Ruzuku ya kati 80,800,000/- Morogoro
11. Morogoro Paralegal Centre (MPC) Ruzuku ya kati 70,800,000/- Morogoro
12 Land Rights Resource and Research Institute Ruzuku ya kimkakati 160,000,000/- Mikoa yote
                                                                                Jumla 903,000,000/-