Hamasa dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia-Arusha Chini

Utangulizi Mradi huu umefadhiliwa na Foundation for Civil Society (FCS) na kutekelezwa na shirika la Tusonge. Mradi uliandaliwa kutumia mbinu mbalimbali ili kupata matokeo tarajiwa. Mbinu zilizotumika ni kama uwezeshaji, mafunzo, mikutano ya kijamii, kampeni za uhamasishaji dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na changamoto wanazokutana nazo makundi maalumu kama wanawake na watoto.  

Hali bora Zaidi kwa Walemavu wa ngozi

Mbinu Kwa ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society, shirika la Caritas limetumia mbinu mbalimbali kuwafikia na kuhamasisha jamii juu ya haki za walemavu wa ngozi na matunzo. Mbinu hizo ni kama mafunzo maalumu, warsha kwa waalimu, wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari. Pia mradi ulitumia klabu za shule kuboresha mazingira ya kujifunza

Tuna furaha tena!

Utangulizi Kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society, taasisi ya Caritas ilitekeleza mradi wa kuhamasisha haki za watu wenye ulemavu wa ngozi. Mradi ulikuwa na mbinu za kusaidia kupunguza changamoto za watu wenye ualbino  katika manispaa ya Tabora. Mradi huu hasa ulijikita katika kutafuta majawabu ya kuduma na sio tu ya muda mfupi kwenye changamoto

Wawezeshwa kujiwezesha

Utangulizi Tanzania League of the Blind (TLB) ambao ni Chama cha watu wenye ulemavu wa macho kiliendesha mradi wa utetezi kwa watu wenye ulemavu. Mradi ulifadhiliwa na shirika la Foundation for Civil Society (FCS) na kutekelezwa wilayani Kwimba kilometa 85 kutoka jijini Mwanza. Pamoja na malengo mengine mradi ulijikita kuwasaidia watu wenye ulemavu kujikwamua na

Hapana kwa ukeketaji!

Kwa kupitia shughuli za utekelezaji wa mradi kwa ufadhili wa Foundation for Civil Society shirika la Tusonge liliibua changamoto zinazosababishwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kufanikisha utatuzi wake. Matokeo yake yamewezesha watendaji wa vitendo hivi hasa mangariba kutoka jamii za wafugaji kutoka kata ya Arusha Chini wilayani Moshi kuacha vitendo hivi na kuwa

Ndoa ya Mitala na Haki ya Wanawake Kumiliki Ardhi

Mara ngapi umeshasikia ndoa ya mitala kama hadithi nzuri kuhusiana na masuala ya haki za wanawake katika jamii? Inawezekana hakuna. Tunaelekea kijiji cha Igula, eneo la Isimani mkoani Iringa kutafiti juu ya familia moja ya kipekee ya mitala. Tumeambatana na  Fatma Tweve na Diana Ndanzi, Mratibu na Afisa Ugani kutoka  Asasi ya kiraia ya TARWOK

Changamoto za Wanawake Kumiliki Ardhi Wilayani Meru

Asasi ya CEDESOTA ilianzisha mradi wa utetezi na ushawishi kwa wanawake  kumiliki ardhi na mali nyingine wilayani Meru mwaka 2016 ukiwa na lengo la kubadilisha mila potofu na imani zinazowabagua na kuwakandamiza wanawake. Mila hizi zinakandamiza mfumo mzima wa maisha ya wanawake na kuwanyima ushiriki katika maamuzi ya familia, jamii na hata umiliki wa mali na

Klabu za kujifunza zasaidia wanafunzi kujikinga na ukatili mkoani Arusha

Kituo cha Centre for Women and Children Development(CWCD) kinatekeleza mradi wa miaka miwili wa‘’Kuzuia na kushughulikia matukio ya ukatili wa kijinsia ‘’unaofadhiliwa shirika la Foundation for Civil Society chini ya eneo la  mila potofu katika kata kumi  za Wilaya ya Arusha Kaskazini mwa Tanzania. Lengo la mradi ni kujenga ufahamu na kushughulikia ongezeko la aina

Umiliki wa ardhi katika jamii za wawindaji, wakusanyaji na wafugaji

Kikundi cha Ujamaa Community Resource Team (UCRT), kilicho fadhiliwa na Foundation for Civil Society , kilianzisha mradi wa miaka miwili wa “Kuhamasisha Haki za kumiliki ardhi za wanawake katika jamii za wawindaji, wakusanyaji na wafugaji”. Katika vijiji vya Lerug, Partimbo, Orkitkit na Amei Wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara. Kwa kupitia Jukwaa la Haki na Uongozi