BODI YA WAKURUGENZI

 

Bodi ya FCS ndio chombo cha pili kwa mamlaka katika taasisi hii. Ndio chombo kikuu cha uangalizi wa masuala yote ya utawala na uendeshaji wa FCS. Majukumu yake ni pamoja na: maamuzi kuhusu mabadiliko yote ya kimuundo ya taasisi, maamuzi yote kuhusu sera na taratibu zote za taasisi, kupitisha mipango ya mwaka na bajeti zote, kujadili na kupitisha taarifa za fedha na wakaguzi wa nje kisha kuziwasilisha kwenye Mkutano Mkuu kwa maamuzi pamoja na kumwajiri na kusimamia utendaji wa Mkurugenzi Mtendaji. Wakurugenzi wa Bodi ya FCS kwa sasa ni: Bw. Sosthenes Sambua (Mwenyekiti), Bi Nesia Mahenge, Bi Joyce Kafanabo na Bw. Frederick Msigalah. Mkurugenzi Mtendaji wa FCS, Francis Kiwanga ni Katibu wa Bodi.

Sosthenes Sambua

 

 

Joyce Kafanabo
Fredrick Msigallah
Nesia Mahenge
Francis Kiwanga
Patrick Maro Kohi
Ally Laay
Munira Hamoud