AINA YA RUZUKU

 

RUZUKU INAZOTOA FCS

 

FCS inatoa ruzuku kwa kazi  gani?

FCS inatoa ruzuku kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zenye umuhimu mkubwa kwa watu maskini na walio pembezoni   katika mgawanyiko ufuatao:

  • Ushiriki wa wananchi na upazaji sauti zao

 

Utawala wa kidemokrasia unawataka wananchi waweze kushiriki kikamilifu katika mambo ya utawala bora na shughuli za demokrasia. Demokrasia pia ina maana kuwa wananchi wanafahamu  taasisi muhimu, haki zao, majukumu na wajibu wao na wanafahamu jinsi ya kushiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo kupaza sauti zao kwa pamoja na kuwafanya viongozi wao wawajibike kikamilifu.

  • Ubora katika sera, sheria na mifumo ya kitaasisi

 

Mojawapo ya tunu muhimu za kijamii  ni kwa jinsi gani mfumo uliopo unavyowahusisha wana jamii kuchangamana na jamii nyingine. Kanuni hii ni muhimu sana katika jamii kwa kuwa inaakisi mfumo wa  utawala bora na pia hukakiksha kuwa haki ya mtu au kikundi ambacho hakipatiwi haki zao kinapatiwa haki hizo. Taasisi ya FCS inawasaidia wananchi wa Tanzania kuitambua hali hiyo na kuimarisha sera, sheria na taasisi ambazo zitawajengea uwezo wananchi , kulinda haki za mtummoja na kuondoa mifumo ambayo inakandamiza na kuzuia ushiriki wa wananchi maskini, vijana, wazee na watu wenye ulemavu na makundi yanayotengwa.

  1. Uwajibikaji katika kufanya maamuzi

 

Uwajibikaji na ufanyaji maamuzi unahitaji serikali  na wadau wasio wa kiserikali kuongeza uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria, kanuni na maadili (kama kupiga vita rushwa)  katika ngazi mbalimbali ikiwemo serikalini, asasi za kiraia na sekta binafsi. Katika kutekeleza hili, masuala muhimu yanayotiliwa maanani ni mafunzo kuhusu Uwajibikaji wa Jamii  na Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma. Kwa hiyo, FCS hutoa matangazo na kuzialika asasi zitakazotekeleza miradi inayolenga (a) Kuwawezesha wananchi kushiriki mchakato wa kupanga mipango na bajeti (kupanga na kutuma rasilimali) na uwajibikaji wa mali ya umma katika matumizi  na uendeshaji wake katika ngazi ya serikali za mitaa na serikali kuu. Mikoa inayolengwa na miradi ya aina hii ni Kigoma, Geita, Kagera, Mwanza na Singida. (b) Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma katika sekta ya elimu ambapo mikoa inayolengwa ni Lindi, Mtwara, Manyara, Tanga na Morogoro. (c) Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha za Umma katika sekta ya maji ambapo mikoa inayohusika ni Kilimanjaro, Dar es Salaam na Tanga.

  • Utoaji wa huduma bora za umma

 

Ukosefu wa utawala bora na uwajibikaji mara nyingi husababisha uzembe na uzorotaji wa utoaji huduma na hivyo kuathiri upatikanaji endelevu wa huduma za jamii kama afya, elimu, na usafi wakiraia na sekta binafsi ili kuimarisha utoaji wa huduma hizo kwa wakati.  FCS hutoa mwaliko kwa asasi zinazotekeleza miradi inayolenga (a) Kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za umma katika sekta za afya na elimu. Msisitizo mkubwa unawekwa katika afya ya mama na mtoto na kuwezesha upatikanaji wa huduma bora kama elimu kwa wasichana  na watoto waishio kwenye mazingira magumu. Mikoa inakotekelezwa miradi hii ni Lindi, Pwani, Kagera na Mbeya.